Rais
Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba,
wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi
matokeo ya Sensa ya watu na makazi.
Bango
linaloonyesha Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika
zoezi la kuhesabu Sensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia
tamati hii leo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo ya Senza ya watu na makazi na
kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya
kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya,
alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa
asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza
nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12,
313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani
Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama
hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012,
ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44,
929,002.
Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
Kikundi
cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa
kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais
Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba,
wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi
matokeo ya Sensa ya watu na makazi.
No comments :
Post a Comment