MCHAKATO wa kuhamisha Kituo cha 
Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi (UBT), kwenda Mbezi Luis 
unatarajiwa kuanza Januari 15 mwaka ujao. 
  
Akizungumzana 
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Jiji Mussa 
Zungiza, alisema lengo la kuhamisha kituo hicho ni kwa ajili ya kupisha 
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART). 
  
Alisema kuhamishwa kwa kituo 
hicho kutakuwa kwa awamu, kutakakokwenda sambamba na kukamilika kwa 
ujenzi wa kituo hicho cha Mbezi. 
  
“Siyo kweli kama ifikapo Januari
 tunahamisha au tunasimamisha shughuli zote pale Ubungo la hasha, 
tutakacho fanya pale tutawakabidhi wajenzi wa mradi huo wa DART ambao 
nao watachagua maeneo maalumu ya kuanzia shughuli zao, huku maeneo 
mengine yakiendelea kutoa huduma bila ya kuleta athari katika utoaji 
huduma”alisema Zungiza. 
  
Zungiza alisema hadi sasa pale Mbezi 
kinachofanyika usafishaji wa eneo hilo la stendi hiyo mpya. Alisema 
katika awamu hiyo ya kwanza watejenga miundombinu ikiwemo uzio, alama za
 kuelekeza magari, njia za kuingia na kutoka. 
  
“Pengine tunatarajia ndani ya miezi mitano tunaamini awamu yakwanza itakuwa imekamilika”alisema. 
  
Zungiza alisema uhamishaji kabisa wa kituo hicho cha Ubungo kutategemea kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kipya cha Mbezi.   
 | 
No comments :
Post a Comment