![]()  | 
Marehemu Amina Singo 
 | 
WAKATI mtangazaji na mwandishi wa michezo
 wa zamani wa Times FM, Amina Singo, akizikwa leo jioni, Shirikisho la 
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko msiba huo 
uliotokea jana.
Msiba
 huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa 
nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya 
kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka 
daima. 
Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.  TFF
 tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na 
marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki 
kigumu cha msiba huo mzito. 
Marehemu
 enzi za uhai wake alifanya mambo mengi katika sekta ya utangazaji na 
muziki kwa ujumla, akishiriki katika kila jema linaloibua na kuendeleza 
maendeleo ya sanaa na michezo nchini.
Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina

No comments :
Post a Comment