Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Hildebrand Shayo 
akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana nakala za kitabu alichotunga 
cha mwongozo wa stadi za namna ya kunukuu maandiko mbalimbali ya rejea kwa kazi 
za kitaaluma. Vitabu hivyo ambayo Kinana naye alivikabidhi kwa Mweyekiti wa 
Umoja wa Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania (TAHLISO)  Paul Makonda, ni kwa ajili 
ya kusambazwa kwenye vyuo mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yamefanyika leo, 
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam. 
Kinana akimkabishi vitabu hivyo Mweyekiti wa Umoja wa Wanafunzi wa vyuo vikuu 
Tanzania (TAHLISO)  Paul Makonda, kwa ajili ya kusambazwa kwenye vyuo mbalimbali 
nchini. Makabidhiano hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, 
Lumumba mjini Dar es Salaam. Picha na Bashir  Nkoromo


No comments :
Post a Comment