MWIMBAJI maarufu wa
muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amewataka
wadau kujitokeza kwa wingi katika tamasha la ‘Shangwe Kagera’ linalitarajiwa
kufanyika Desemba 9 kwenye Ukumbi wa Linas mjini Bukoba na uwanja wa Kaitaba.
Muhando na Enock Jonas
‘Zunguka’ watapamba katika maalum la kuchangia watoto yatima lenye lengo la kuielimisha
jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha
magumu.
Akizungumzia tamasha hilo
Rose alisema amejiandaa kusherekea Uhuru
kwa aina yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto
yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
“Nimefurahi kupata nafasi ya
kutumbuiza katika tamasha hili la aina yake hasa katika mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara ya kwanza
kuonekana live katika mji wa Bukoba”, alisema .
Muhando aliwamba wananchi wa
Bukoba kufika kwa wingi katika tamasha hilo la kipekee katika ukuonyesha moyo
wa upendo kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
Alisema kupitia tamasha hilo
anatarajiwa kuwapa uhondo wa nyimbo zake za zamani sambamba na kutambulisha
nyimbo zake mpya ambapo wakazi wa huko watapata fursa ya kuzisikiliza kwa mara
ya kwanza.
Naye Zunguka amewataka wakazi wa Kagera kukaa mkao
wa kula kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie kupata burudani ya kutosha na ya
kipekee kutoka kwake ambayo itawajenga
roho ya imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika
mazingira magumu ili nao waweze kufaraia maisha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha
hilo,Melkizedeck Mutta alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kuwataka wadau
kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
No comments :
Post a Comment