Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania 
Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa akisungumza na waandishi wa habari 
(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kinywaji kipya kinachoitwa 
ZANZI (kinachoonekana pichani) iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar 
es Salaam leo.

 Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania 
Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe akitoa ufafanuzi wa Kinywaji hicho 
kipya aina ya ZANZI ambacho kinapatikana katika ujazo wa 750ml na katika Pakiti 
zenye ujazo wa 100ml ambacho kitakuwa kikipatikana nchi nzima.Katikati 
ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TDL,David Mgwassa na kulia ni Meneja 
Usafirishaji wa TDL,Bavon Ndumbati.
 "...hiki ndicho kinywaji kipya tulichokizindua 
leo..." 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania 
Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa (katikati),Meneja Masoko wa Kampuni ya 
Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe na Meneja Usafirishaji 
wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Bavon Ndumbati wote kwa pamoja 
wakigonganisha glass kuashiria uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho uliofanyika leo 
kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam




No comments :
Post a Comment