Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal 
na mkewe Mama Asha Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati
 alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya 
Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba 23, 2012. Mzee huyo 
anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 13.
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na
 wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo 
Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa 
ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal.
 Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.
  Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, 
Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo 
cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akipokea ramani ya ujenzi mpya wa shule ya Chwaka, kutoka kwa Mwalimu 
Mkuu wa shule hiyo, Fadhili Hamada Mshamba, wakati alipotembelea 
kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) 
leo.
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal 
na mkewe Mama Asha Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya 
Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya 
kituo hicho leo.
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal 
na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mzee Silima Jendele, wakati 
Makamu alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Wazee leo, katika Mkoa 
wa Kusini Unguja.
PICHA ZOTE NA OMR

No comments :
Post a Comment