Baraza la
sanaa la aifa limeteuwa majina matatu kati ya sita ya majaji yaliopendekezwa na waandaji wa shindano la kumsaka mwanamitindo
wa mwaka mwenye sifa za kipekee.
Uteuzi huo
wa wabunfu Asia Idarous
khamsini,Gymkhana Hilall (paka wear) na Martin Kadinda umefanyika mwishoni mwa
wiki hii baada ya baraza la sanaa la
Taifa (Basata) kupitia wasifu wao na kuridhika wawe waamuzi rasmi wa shindano
la Unique model 2012.
Kinyang’anyiro
cha kumsaka mwanamitindo huyo wa mwaka kinajumuisha washiriki kumi na mbili
katika jukwaa moja ambapo fainali hizi zitafanyika tarehe 28 desemba katika
ukumbi wa maraha New Maisha club ulioko Oysterbay jijini Dar.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Methuselah Magese amesema
kuwa maandalizi ya shindano hilo yako vizuri sana na washiriki wamenorewa kiasi
cha kutosha imebaki ni kazi ya umatiwa wapenzi wa mambo ya mitindo kujitokeza
kwa wingi kushuhudia nani atachukua taji siku ya ijumaa.
Shindano la
unique model litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa ikiongozwa na rapa
maarufu Chalz Baba ikiambatana na ngoma za asili toka kwa Costa Siboka na
utambulisho wa msanii mkali wa bongo flava B-shop kwa mara kwanza atatoa
burudani ambayo haijawahi kutokea.
Magese
aliongeza kuwa mbali ya burudani kutakuwa na zulia jekundu(Red carpet) kwa watu
maarufu na watu waliopendeza zaidi siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa ni Tshs
15,000 tu kiingilio ambacho hakitengi tabaka la watu flani katika jamii.
No comments :
Post a Comment