Kwa maelekezo ya ITU kwamba
huduma za televisheni za utangazaji kubadili kutoka Analojia na kwenda
katika mfumo wa digitali kabla ya Juni 17, 2015, lakini kwa nchi ya
Tanzania tarehe ya mwisho ya kubadili mfumo ni Desemba 31, 2012.
Ili kuwa na uwezo wa kutekeleza
mabadiliko haya katika wakati, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
imeunda kampuni ya Ubia na kampuni ya Star Communication Network
Technology Co. LTD ya China, inayojulikana kama Star Media (Tanzania)
LTD inayotumia jina la kibiashara la STARTIMES. wajibu wa Kampuni hii
ya Ubia na ya kisasa, ni kuleta mapinduzi katika huduma za televisheni
na utangazaji kwa njia ya digitali na kutoa huduma za multiplex katika
Tanzania. STARTIMES tayari imeshabadili na kuingiza katika mifumo ya
digitali mikoa saba katika Tanzania Bara yaani Mwanza, Mbeya, Dodoma,
Arusha, Moshi, Tanga na Dar es salaam. Kufikia mwisho wa mwaka
huu,kabla ya kubadili rasmi mfumo mkoa wa Morogoro pia utaunganishwa
katika mfumo wa digitali kama miko tajwa.
Inatarajia pia kujenga Kituo
cha kurushia cha kisasa katika eneo la Makongo kilimani ili kuboresha
signal/urushwaji wa matangazo yetu katika Mkoa wa Dar es Salaam na
baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani.
Kampuni ya Star Time vile vile
inakusudia kubadili Zanzibar na tayari tumepata leseni kwa ajili ya
kujenga kituo cha televisheni na kupeleka huduma za mfumo wa digitali
kabla ya tarehe ya kubadili (Switch –off) kama kila kitu kitakwenda
kulingana na mipango yetu. Hata hivyo, mpango wetu ni kwamba Tanzania
nzima lazima kubadilishwa kwenda kwenye mfumo wa digitali mapema
iwezekanavyo ili kila Mtanzania anaweza kufurahi ulimwengu wa digitali.
No comments :
Post a Comment