Meneja Mawasiliano wa TCRA, Bw. Innocent Mungy alisema jana kuwa siku ya mwisho ya watanzania kutumia analojia itakuwa Desemba 31, mwaka huu.
"Vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko ya kutoka Analogia kwenda digitali ni miaka miwili na nusu, hata Rais Kikwete alipozindua nembo ya digitali, tumezunguka nchini nzima kutangaza"alisema Bw. Mungy.
Akihojiwa katika kipindi cha luninga cha Star juzi, Bw. Mungy alisema mitambo ya analojia itazimwa Desemba 31 na watakaoendelea kutumia luninga zao ni wale wenye ving'amuzi.
"Wananchi wote tunawatoa wasiwasi kuwa wasitupe televisheni zao za zamani kwa vile zinaendelea kutumika wanachotakiwa kufanya ni kununua ving'amuzi kutoka katika kwa mawakala waliosajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano" alisema Mungy.
Alisema muda huo hautaongezwa na kwa vile imechukua muda mrefu kutoa elimu kwa watanzania Serikali haitakuwa na malalamiko kutokana na kuzimwa kwa mitambo hoyo.
Watu wengi nchini wameingiwa na hofu kuhusu kupata mawasiliano katika televisheni zao baada ya kumalizika kwa muda wa kutumia analojia ambao unatumika kwa watanzania wengi ambao hawana ving'amuzi.
No comments :
Post a Comment