Wapendwa ndugu, jamaa na marafiki
popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012, ambao kwa
hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha, dhoruba za hapa na pale
wengi zilitukumba, lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono
akatuinua na maisha yakaendelea.
Binafsi mpaka dakika hii namshukuru
Mungu nikiwa mwenye afya njema kabisa. Maisha ya sasa Wanadamu wengi
wamekuwa dhaifu kwa mambo mengi, lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa
kumtumia katika sala zako kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia. Yako
mengi ambayo naweza nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia. Nasema
asanteni kwa ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine, kama
kuna mahali nilikosea, tukakwaruzana kidogo basi "NAFSI NI NYONGE"
Tusameheane na maisha yaendelee.
Tunahamia mwaka mwingine mpya kabisa
2013, basi na tuendelee na ushirikiano huu tuliokuwa nao kwa mambo
mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika maisha yetu, Mwaka 2013
uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia kwenye mfumo wa kidijitali,
tushauriane, tuelemishane tunyooshane njia iliyo sahihi ili kila mmoja
kila wakati abaki nafsini mwake mwenye furaha daima, Pia tumtangulize
Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia azidi kuzibariki kazi za mikono
yetu daima.
Kwa Blogaz wenzangu, changamoto
nyingi tumekumbana nazo 2012, ikiwemo tatizo kuu la KUKOPY NA KUPASTE.!
Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua kwa namna moja ama nyingine,
basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia ufumbuzi, kama si kuzimaliza
kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza ili kuzimaliza kabisa, huku
suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao kuu ya mabadiliko miongoni
mwetu. Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha tuna uwezo mkubwa wa
kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia kwa namna moja ama
nyingi, basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano huu hauteteleki ama
haupotei kirahisi, badala yake tuiimarishe zaidi kila kona.
Natoa shukurani za dhati kabisa kwa
makampuni na wadau mbalimbali ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango
mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele na libeneke hili , si vibaya
nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti Breweries Ltd, Airtel,
Bayport, Msama Promotions Ltd, kampuni ya R&R, Dada Teddy Mapunda,
Hoyce Temu, Blogaz wote (bila kinyongo) na wengine waliotupa hatua ya
kusogea kwa namna moja ama nyingine, Mungu awabariki sana.
Asanteni
Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.
No comments :
Post a Comment