Ridhiwani Kikwete.
Assah Mwambene |
MAANDALIZI
ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) yanaenda vizuri na wajumbe wanatarajiwa kufika Bagamoyo Ijumaa
Desemba 28, 2012 mchana kwenye hoteli ya Kiromo View Resort watakapolala
na kufanyia mkutano.
Ijumaa
hiyo washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria Bagamoyo na
jioni kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya TASWA FC na
Bagamoyo Veterani itakayofanyika Uwanja wa Mwanakalenge na usiku
wajumbe watakuwa na chakula cha pamoja na kubadilishana mawazo kuhusiana
na masuala mbalimbali yahusiyo michezo na taaluma ya habari.
Mkutano
Mkuu utafunguliwa Jumamosi Desemba 29, saa tatu asubuhi na mgeni rasmi
atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu za Taifa za Vijana,
Ridhiwani Kikwete.TASWA imechukua jukumu la kumualika kutokana na kuwa
mdau mkubwa na rafiki wa chama chetu.
Mkutano
utafungwa jioni ya siku hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Assah Mwambene ambaye hiyo pia itakuwa nafasi nzuri kwake
kuweza kuzungumza na wana habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya
kitaaluma.
Katika
mkutano huo wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili
Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na
masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo na
maendeleo ya michezo kwa ujumla Pia
kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo,
ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama
ambayo nayo itajadiliwa kwenye mkutano huo.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze
kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini
imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya
jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo litakuwa kama
ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye mkutano wetu.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
No comments :
Post a Comment