Ofisa
Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Bi Stella Vuzo akiwakaribisha waandishi wa chama cha habari za
Mazingira Tanzania (JET) na kuwatambulisha wazungumzaji katika mkutano
wa taarifa fupi katika kuwapa mwanga kuhusu yatokanayo na taarifa ya
mabadiliko ya tabianchi uliofanyika Doha. Katikati ni Mtaalam wa
Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro na kushoto Mkurugenzi Msaidizi wa
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
Mkutano
huu uliowakutanisha pamoja waandishi wa habari za Mazingira Tanzania
(JET) umeratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini
(UNIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo.
Mtaalam
wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akielezea kwa ufupi jinsi Umoja
wa Mataifa unavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupambana na
mabadiliko ya Tabianchi na kufafanua Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa
Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa
nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi
akizungumzia yatokanayo mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo swala
la Gesi joto ambapo amesema kwa nchi kama Tanzania haichafui mazingira
kulinganisha na nchi zinazoendelea zenye viwanda vikubwa pamoja na
makubaliano waliyofikikia katika mkutano huo ambayo yatatolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira hivi karibuni.
Mmoja
wa waandishi wa habari Bi. Judica Laswai kutoka TBC akieleza namna
alivyoweza kupata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa mabadiliko ya
tabianchini uliofanyika Doha hivi karibuni kwa kushiriki mashindano ya
kuaanda vipindi vya mazingira na mwishowe kushinda safari iliyodhaminiwa
ni Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) ambapo
amewahimiza wanahabari wenzake kutumia fursa za mitandao ya kijamii.
Pichani
Juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari za Mazingira (JET)
wakiuliza maswali na kutoa maoni kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa Mazingira (JET) waliohudhuria mkutano huo.
Ofisa
habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
Bi. Usia Nkhoma akitoa changamoto kwa waandishi wa habari wa mazingira
kuzipa kipaumbele habari za mazingira na kuwataka kuweka usawa katika
habari wanazoandika.
No comments :
Post a Comment