Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na
vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na
wananchi mbali mbali waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika
uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku mbili.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara
ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi za ADC
zilizorejeshwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho na kujiunga na CUF
katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya
Tangamano Jijini Tanga.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
----
Chama
Cha Wananchi CUF kimesema kuwa amani ya kudumu haiwezi kupatikana
katika nchi yoyote bila ya kuwepo haki na usawa katika jamii.
Amesema
miongoni mwa sera za msingi za chama hicho ni kuwaunganisha wananchi,
na kwamba umoja hauwezi kupatikana kwa kuendeleza sera za kibaguzi na
kutowatendea haki wananchi.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa CUF na wakaazi wa jiji la Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa CUF na wakaazi wa jiji la Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
“Kila
mtu ana haki sawa na mwengine kikatiba na kila mtu anastahiki
kuheshimiwa haki zake, kwa hivyo nasema tena kuwa popote penye ubaguzi
hapawezi kuwa na umoja”, alisisitiza Maalim Seif.
Katika
Mkutano huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar amewatanabahisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya kazi ya
kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, na kuacha kushabikia masuala ya
kisiasa.
“Kikatiba
viongozi hawa si wanasiasa bali ni watumishi wa umma, lakini cha
kushangaza bado wapo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanajifanya wakereketwa wa
vyama fulani na kuwabagua wananchi”, alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
Amewapongeza
viongozi wa Mkoa wa Tanga kwa kuweka kando tofauti za kisiasa na
kushirikiana na wananchi katika kusogeza mbele maendeleo ya Mkoa huo.
Mapema
Mkuu wa Wilaya ya Tanga bibi Halima Dendegu ambaye alipanda jukwaani
kuwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano huo, amesema uongozi wa Mkoa
huo unashirikiana vizuri na wananchi na wanaishi kwa kupendana na
kuheshimiana.
Akizungumzia
kuhusu uchumi, Katibu Mkuu wa CUF amesema chama hicho kina sera imara
za kujenga uchumi wa Tanzania kwa lengo la kuwakomboa Watanzania
kuondokana na hali ngumu ya maisha.
Amesema
Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bado hazijatumika
ipasavyo kuweza kuwanufaisha watanzania, na hivyo kuendelea kubakia
kuwa nchi maskini.
“Ardhi
ya Tanzania ina rutba nzuri ambayo takriban inakubali kila aina ya
mazao, tuna bahari ambayo nayo ina rasilimali kadhaa wa kadhaa, madini
ya kila aina, Tanga kuna bandari na kadhalika, lakini wapi bado
rasilimali hizi zinatumika kuwanufaisha watu wachache na makampuni ya
kigeni na sisi Watanzani wengi tulio maskini tunabakia kushuhudia
mashimo tu”, alifahamisha Katibu Mkuu wa CUF.
Amesema
iwapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015,
kitahakikisha kuwa wananchi wananufaika moja kwa moja na rasilimali za
nchi, na kwamba robo ya mapato yatokanayo na rasilimali hizo yatatumika
kulipa madeni ya nje ambayo yameripotiwa kufikia shilingi trilioni
ishirini (20).
Akizungumzia
kuhusu maendeleo ya chama hicho, Maalim Seif amesema chama bado kiko
imara na wala hakitoyumba kutokana na kujengwa na misingi ya imara.
“Watakaojaribu
kukibomoa watashindwa, CUF hakiwezi kusambaratika hata siku moja kwa
kuwa kimejengwa kwa misingi imara na viongozi wake wako imara na
madhubuti kabisa”. Alifahamisha.
Katika
risala yao wafuasi wa CUF Mkoa wa Tanga wameeleza kuwa changamoto kubwa
inayowakabili kwa sasa ni upungufu wa dawa pamoja na kuharibika mara
kwa mara kwa X-ray katika hospitali ya rufaa ya Bombo Mkoani humo.
Nae
Naibu Mkurugenzi wa haki za binadamu na mawasiliano ya umma wa CUF bw.
Abdul Kambaya amesema rasilimali zilizopo Tanzania zinatosha kuwakomboa
wananchi na umaskini, lakini mfumo wa uongozi uliopo bado haujazingatia
maslahi ya umma na unalenga kuwanufaisha watu wachache.
“Bandari
ya Tanga haifanyi kazi vizuri, reli ya Tanga imekufa, mashamba ya
mkonge yamekufa, tujiulize watu wa Tanga kuna nini?” alihoji Kambaya na
kudai kuwa limetokana na mfumo uliopo wa uongozi.
Katika
Mkutano huo Chama hicho kimepoa kadi ishirini (20) za wafuasi wa Chama
Cha ADC walioamua kujiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.
No comments :
Post a Comment