Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala 
Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane 
Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na 
Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa 
watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho 
atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni 
Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)
 Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi 
ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima 
na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa 
mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya 
shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.
Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa 
akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya
 kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika
 kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.
Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka 
mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa 
wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.
Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa 
chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio 
Katika Mazingira Hatarishi  cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund 
ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.
Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s 
Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka
 huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.
No comments :
Post a Comment