Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia
yatazimwa rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28
mwakani ili kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.
Waziri
wa habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema
hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa
Habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya
kuhamia katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.
Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya
Utangazaji Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu
ambapo kwa zoni ya Zanzíbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe
mwisho rasmi wa matangazo ya Analogi.
Waziri
Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi
ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo
ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST
hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.
Akizungumzia
matayarisho ambayo yamefanywa na Wizara yake katika kuukabili mfumo
mpya wa Matangazo ya Dijitali Waziri Mbarouk amesema tayari wamejenga
kituo cha usambazaji ishara(signals) katika eneo la Rahaleo
kitakachokuwa na kazi ya kupokea na kusambaza ishara na mitambo ya
uendeshaji.
No comments :
Post a Comment