Amir Mhando Katibu Mkuu TASWA
20/07/2012
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
(A) AJALI YA MELI ZANZIBAR
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa
Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutokana na vifo vilivyotokea vya
watu zaidi 60 baada ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit juzi eneo la kisiwa
cha Chumbe,Zanzibar.
TASWA
inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu, huku tukiwaombea
waliofariki Mwenyezi Mungu ahifadhi roho zao mahali pema na wale
majeruhi awape nguvu wapone haraka waweze kuendelea na shughuli zao za
ujenzi wa Taifa.
Tunaziomba
familia zilizopoteza ndugu zao ziwe na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu na waamini kwamba huo ni msiba wetu sote na si wao peke yao.
TASWA
inaamini wapo wanamichezo waliopoteza maisha kwenye meli hiyo na pia
wapo wanamichezo waliopoteza ndugu na jamaa zao, wote tunawapa pole na
wawe na moyo wa subira.
(B) MKUTANO MKUU WA MWAKA
Kamati
ya Utendaji ya TASWA inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo
mengine kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya chama hicho ikiwemo
kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa mwaka.
Awali
sekretarieti ya TASWA ilipendekeza mkutano huo uwe mwanzoni mwa Agosti,
lakini ili kuepuka kuingiliana na mwezi mtukufu wa Ramadhan mkutano huo
sasa utafanyika mwishoni mwa Agosti katika tarehe na ukumbi ambao
utapangwa na Kamati ya Utendaji.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/07/2012
No comments :
Post a Comment