DAR ES SALAAM, Tanzania
JUMUIYA
ya Wazazi nchini imesema itahakikisha inarudisha mali zake zote zilizovamiwa
kinyume cha sheria ikiwemo Shule ya Kaole ambayo ni ya kihistoria kati ya nchi
ya Msumbiji na Tanzania.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,
Abdallah Bulembo alisema huo ni mkakati wa uongozi mpya uliyoingia madarakani
hivi karibuni.
Alisema
kitendo alichofanya Mkurugenzi wa shule za Green Acle, Julian Bujugo
hakikubaliki kwani kimevunja mikatiba ya nchi mbili ya kulifanya eneo hilo
kuendelea kuwa la kumbukumbu ya wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji.
“Haitafika
Januari mwaka ujao Shule ya Kaole itakuwa imeisharudishwa mikononi mwa Jumuiya
kwani shule ile ni ya nchi mbili naitaendelea kuwa ya kumbkumbu ya
FLELIMO”alisema Bulembo.
Bulembo
alisema eneo la Kaole haliwezi kuuzwa na kumilikiwa na watu wengine na baadala
yake litabaki kuwa la watu wa msumbiji kutokana na ukweli kwamba kuna makaburi
ya ndugu zaao ambapo hutembelea eneo hilo mara kwa mara.
“Tumemuita
Bujugo kesho tukutane naye na kumjulisha kuwa alichofanya ni ukiukaji wa sheria
hivyo anapaswa kuanza mchakato wa kukabidhi shule hiyo haraka kwa
jumuiya”alisema.
Akifafanua
zaidi, Bulembo alisema Jumuiya hiyo ilikumbwa na matatizo mengi hapo awali
kutokana na baadhi ya watendaji kutokuwa waaminifu kuuza baadhi ya mali.
Alisema
baada ya uongozi mpya kuyabaini hayo, inawatahadharisha wale wote waliyovamia
mali za jumuiya hiyo kutambua kuwa wakati umefika kwa kuzirudisha hata kama ni
kwa fidia kidogo watakayopewa na Jumuiya kinyume chake watawaburuza mahakamani.
Akizungumzaia
maendeleo ya shule za jumuiya hiyo, Bulembo alisema zipo shule 71 ambapo kati
hizo, 53 zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma.
Alisema
kutokana na hali hiyo wamefikia muafaka na Kamati ya Shule hizo kuanza mchakato
wa kuzibadili zile 18 ambazo hazifanyi fizuri
kuwa za ufundi (VETA), ambapo alisema Veta yao itakuwa tofauti kwani
itapokea vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na siyo kidato cha nne, kwani
kundi hilo linasahaulika pindi liingiapo mitaani.
“Niwatowe
wasiwasi wazazi wenzangu kuwa Jumuiya haina mpango wa kuuza baadhi ya shule
zake zinazofanya vibaya bali mpango wetu ni kuziimalisha kiufundi ili ziweze
kupokea kundi hilo la watoto wetu wanaomaliza elimu ya msingi” alisema Bulembo
Vilevile
alisema kuwa hivi sasa shule zao siyo za huduma tena bali zitakuwa za
kibiashara kama nyingine kwa sababu sera zilizoanzisha shule hizo awali
zimepitwa na wakati.
No comments :
Post a Comment