Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, October 19, 2009

MENEJA WA UWANJA WA UHURU AFARIKI DUNIA

Kaimu katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bw. Gasper Mwombezi akizungumza na wandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo alipotangaza kifo cha Ghafla cha Meneja wa viwanja vya Uhuru na uwanja mpya wa Taifa kilichotokea usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na ukuta.
Masanja alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili ambapo baadae alifariki Dunia Bw. Gasper amesema habari zaidi zitatolewa baadae lakini Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo imeunda kamati ili kushughulikia masuala yote kuhusiana na msiba huo.
Selestin Masanja alizaliwa Urambo Mkoani Tabora Januari 20 mwaka 1957 na kusoma katia elimu ya msingi hapo baadae alijiunga na shule ya Sekonsari ya Itagana 1972-1975 baadae shule ya Sekondari Minaki 1975-1977.
Mwaka 1988 alienda nchini Cuba katika jiji la Havana na kuchukua shahada ya Uzamili wa Physical Education.
Akiwa mfanyakazi wa Serikali katika idara yaMichezo Marehemu Massanja aliwahi kuwa Afisa michezo mkuu daraja la I, Meneja wa uwanja wa Taifa, Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya TFF, Katibu mkuu wa FAT Msaidizi, Afisa michezo idara ya Michezo, Katibu mkuu msaidizi wa FAT tena Kocha Mkuu wa African Sport ya Tanga

No comments :

Post a Comment