
Tukianza kunako uwanja wa Uhuru Mnyama Simba ambaye ameweka kambi huko visiwani Zanzibar anatarajiwa kuwasili jijini kesho asubuhi kwa ndege tayari kwa mchezo huo na kisha kurejea kuendelea na mawindo dhidi ya Yanga hapo Oktoba 31.
Akizungumza na michezo Afisa habari wa klabu ya Simba Cliford Mario Ndimbo amesema wamefikia hatua ya kukodi ndege kufuatia ratiba ya mazoezi ya mwalimu kwa vijana hao wa msimbazi ambao hawajapoteza hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi kuu.

Wakati mashabiki wengi wengi wa kandanda jicho lao likiwa katika mchezo wa Simba na Azam Fc, klabu ya African Lyon imekiri ligi kuwa ngumu na kutamba wanauhakika wa kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya Majimaji.
No comments :
Post a Comment